Balozi wa Tanzania Nchini Korea Kusini. Balozi Togolani Edriss Mavura, ameshiriki Mkutano wa Mwaka wa Jukwaa la Biashara la Afrika na Korea ( 2021 KOREA - AFRICA BUSINESS FORUM), ulioandaliwa na Shirika la Korea Afrika Foundation kwa ushirikiano na Wizara ya Mambo ya Nje ya Korea uliwakutanisha viongozi wa Kampuni za Kibiashara za Korea, Mabalozi wanaowakilisha nchi zao nchini Korea, Umoja wa Afrika (AU) na Wadau wengine wa Maendeleo.

Mkutano huo umejadili namna bora ya ushirikiano kati ya Korea na Afrika baada ya Kuanza kwa utekelezaji wa Mkataba wa Biashara wa Bara la Afrika  ( AfCFTA). 

Mkutano huu umejadili namna nchi ya Korea itakua mshirika mzuri kwenye masuala ya ujenzi wa miundombinu, biashara, viwanda na nishati salama.

Kwa upande wake Mhe. Balozi ametumia Mkutano huo kukutana na wadau mbalimbali wa maendeleo ambao wameonesha nia ya kuja kuwekeza Tanzania kwenye sekta ya madini.

  • Balozi wa Tanzania Nchini Korea Kusini. Balozi Togolani Edriss Mavura, ameshiriki Mkutano wa Mwaka wa Jukwaa la Biashara la Afrika na Korea 2021Balozi wa Tanzania Nchini Korea Kusini. Balozi Togolani Edriss Mavura, ameshiriki Mkutano wa Mwaka wa Jukwaa la Biashara la Afrika na Korea 2021